Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ndugu Ismail Ali Ussi, leo tarehe 3 Juni 2025 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mzinga kilichopo Mtaa wa Magore, Kata ya Mzinga, Jimbo la Ukonga Jijini Dar es salaam
Mradi wa ujenzi kituo cha afya Mzinga unatekelezwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani, unakadiriwa kugharimu jumla ya Shilingi 3,706,197,163.95, ambapo hadi Mei 2025, kiasi cha Shilingi 1,565,000,000 kimepokelewa na Shilingi 1,225,532,876.82 zimetumika.
Mradi huu unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wapatao 500,000 kutoka kata tano za Mzinga, Kivule, Kitunda, Kipunguni B na Msongola. Kupitia kituo hiki, huduma za afya zitasogezwa karibu na wananchi na kupunguza umbali wa kufuata huduma za dharura,
Akiongea mara baada ya kuweka jiwe la msingi kiongozi wa mbio za Mwenge Ndugu Ismail Ussi amesema
“Kuweka jiwe la msingi leo ni ishara kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kusogeza huduma muhimu kwa wananchi na kuimarisha ustawi wa jamii,” amesisitiza Ndugu Ismail Ussi
Kituo cha Afya Mzinga kimebeba matumaini mapya kwa wakazi wa Ukonga na maeneo ya jirani, na kinategemewa kuwa nguzo ya huduma bora za afya katika Jiji la Dar es Salaam.
KAULI MBIU “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa Utulivu na Amani”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.