-Ataka uwepo wa Mawasiliano kisekta katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
-Asisitiza utatuzi wa kero za wananchi
-Hamasa ya kujitokeza kupiga kura tarehe 29 Oktoba iendelee
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Abdul Rajabu Mhinte amefanya kikao Cha Robo ya Nne ya Mwaka 2024/2025 na Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Karimjee
Katika kikao hicho RAS Mhinte alisisitiza suala la utoaji wa huduma Bora kwa wananchi jambo ambalo ni matamanio na mategemeo yao . “Nchi imekua kiuchumi kwa sasa na maendeleo mengi yamepatikana kwa sababu ya uwajibika unaofanyika na kupelekea jamii ya wana-Dar es Salaam kupata huduma Bora” Alisisitiza RAS Mhinte
Hata hivyo, Katibu Tawala alitaka uwepo wa Mawasiliano kati ya Taasisi Moja na nyingine ili kuleta ufanisi mzuri wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuepuka matatizo au changamoto zozote zinazoweza kujitokeza
Vile vile RAS Mhinte alisisitiza kero za wananchi kusikilizwa na kutatuliwa mara Moja. Wananchi wanapaswa kusikilizwa na kuhudumiwa kwa lugha nzur ili watoke wameridhika na huduma walizozipata
Hata hivyo, Katibu Tawala ameongeza kuwa Hamasa ya wananchi kujiandikisha kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 inapaswa kuendelea kwani huu ni mwaka wa uchaguzi, kwa namna walivyojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ndivyo hivyo wanapaswa kwenda kupiga kura
Ikumbukwe kuwa katika kikao Cha Robo ya Nne ya Mwaka 2024/2025 Watendaji wa Taasisi za Umma za Serikali waliwasilisha taarifa zao za mwaka wa fedha ulioisha.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.