Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila, amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam zinapaswa kuanzisha timu za mpira wa miguu ili kuibua vipaji na kutoa ajira kwa vijana, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya michezo nchini.
Mhe. Chalamila ametoa agizo hilo leo, Septemba 22, 2025, katika hafla ya kukabidhi magari kwa Wakuu wa Wilaya za Kigamboni, Ubungo pamoja na golikipa wa Timu ya Tanzania Taifa Stars na Simba Yakoub Suleiman, iliyofanyika Kinondoni jijini humo.
Amesema kuwa tayari Wilaya ya Kinondoni ina timu yake ya KMC, hivyo ni wakati sasa kwa Halmshauri nyingine, ikiwemo Halmashauri ya Jiji kujifunza na kuiga mfano huo.
“Jiji hili linakusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 300, hivyo ipo sababu ya kila Halmashauri kuanzisha timu yake. Michezo ni biashara, utalii na burudani. Hivi sasa utambulisho wa Mkoa wetu ni timu ya KMC, ambayo haitambulishi Kinondoni pekee bali Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla,” amesema Chalamila.
Aidha, amewataka Maafisa Michezo kushirikiana na Wakuu wa Wilaya katika kuanzisha timu hizo sambamba na kumbi za mchezo wa ngumi, kama ambavyo tayari kumeanzishwa Kinondoni.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.