Kila Tarehe 08 Machi Taifa linaadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambapo Leo Machi 08, 2023 maadhimisho hayo katika Mkoa wa Dar es Salaam yameweza kuadhimishwa katika viwanja Vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla.
Katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo "UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA NI CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA" yameweza kubeba sura ya Kongamano la Wanawake na Fursa za Kiuchumi, yaliwapa nafasi kina mama na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali kushiriki, kuonyesha bidhaa zao, na kuuza bidhaa hizo.
Akiongea katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla amesema “Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muunguno wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwawezesha Wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri kwani Billioni 13.9 zimeweza kutolewa kwaaajili ya kusaidia vikundi vya Wanawake,Vijana pamoja na watu wenye ulemavu ikiwa bilioni 6.1 wamepewa Wanawake huku bilioni 5.9 zikielekezwa katika vikundi vya Vijana na bilioni 1.8 zikielekezwa katika vikundi vya watu wenye ulemavu ambapo takribani vikundi 1243 vimeweza kunufaika na mikopo hiyo ikiwa vikundi 69 ni vya wanawake vukundi 428 ni za vijana na vikundi 126 vikiwa ni vya watu wenye ulemavu hivyo natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam mjitokeze kwa wingi kunufaika na fursa hii ya mkopo wa asilimia 10%ya mapato ya ndani ya Halmashauri ili muweze kujikwamua kiuchumi pia kwa wale ambao mshapata mikopo hiyo mhakikishe mnarejesha fedha hizo kwa wakati ili wengine nao waweze kupata mkopo.”
Aidha Mhe Makalla ameendelea kusema “Mimi kama kiongozi wa Serikali nimeona niwaoneshe kwamba ninaheshimu Wanawake na kuthamini juhudi zao wanazozifanya kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ambapo leo hii duniani kote wanaadhimisha siku ya Wanawake kama sisi Tanzania ambapo kitaifa hufanyika kila baada ya Miaka mitano, na Kila Mwaka kila Mkoa hufanya katika Mkoa wake lengo likiwa kuwawezesha Wanawake kujikwamua Kiuchumi, kielimu,kiafya pamoja na kuwawezesha wajasiriamali.”
Sambamba na hilo Mhe. Makalla ameweza kuzishukuru Taasisi, Mashirika na Makampuni binafsi ambayo yameweza kuwaruhusu wanawake kuweza kuungana na wanawake wengine siku hii ya leo niwaase Wanawake kuwa wamoja katika kutetea haki zenu na Taifa letu kwa ujumla na ndio maana hata mimi nimeheshimu siku hii nakuweza kuungana na ninyi.
Vilevile Mhe.Makalla aliweza kukagua mabanda ya wajasiriamali kutoka Halmashauri zote zaMkoa wa Dar es Salaam ambao ni wanufaika wa Mkopo wa asilimia 10% za mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo aliweza kujionea bidhaa mbalimbali wanazotengeneza wanawake wajasiriamali huku akitoa rai kwa wanawake kuhakikisha wanapata mafunzo ili waweze kupata Masoko ya ndani na nje, “Kadri uchumi unavyokua fursa zinazidi kuongezeka hivyo naamini kwa mikono ya Wanawake, Masoko tunayo hivyo nitoe wito kwa wanawake wathibiti ubora wote kuwatia wanawake wengine moyo tusiwakatishe tamaa ili waweze kukua kiuchumi pia nitoe wito kwa Jamii kujenga tabia ya kununua bidhaa zinazozalishwa kwa mikono ya wajasiriamali wenzetu na pia wajasiriamali mhakikishe mnatengeneza bidhaa zinazokidhi ubora na viwango ili muweze kupata Masoko ndani na nje ya nchi.” Amesisitiza Mhe. Makalla.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ambaye ni mwenyeji katika maadhimisho haya yaliyofanyika katika Wilaya ya Ilala amesema “Kwa niaba ya Wakuu wenzangu wa Wilaya Nyingine nipende kuwapongeza wamama wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam ambao wameweza kujiajiri kupitia mkopo wa Asilimia 10% za mapato ya ndani ambapo hii leo wameweza kutambulisha bidhaa zao hivyo nipende kukushukuru Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam kwa kuungana na Wanawake hawa katika Siku yao hii Muhimu pia nikuhakikishie wakani Mimi na Wakuu wa Wilaya wenzangu tutafanya jambo kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake hawa wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam kujikwamua Kiuchumi.”
Akiongea kwa niaba ya Vikundi vya Wajasiriamali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 %ya Halmshauri mjasiriamali wa Kikundi cha wethy kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bibi.Letisia Pius Rutta amesema “Tunaishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapindunzi na Sera mbalimbali hasa kumuinua Mwanamke Kiuchumi ameweza kutupatia mikopo na kuanzisha majukwaa mbalimbali yanayotetea haki za Wanawake hivyo tunamuahidi tutatumia fursa hii kujikwamua Kiuchumi.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.