Katika kuendeleza Kampeni ya Usafi 'Safisha, Pendezesha Dar es Salaam' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla leo tarehe 29 Aprili, 2023 ameshiriki zoezi la usafi katika kata ya Ilala ambapo usafi huo hufanywa kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi huku akiwataka viongozi wote wa Masoko huhakikisha wanasimamia usafi masokoni hasa kipindi ichi cha masika ili kuhakisha Wananchi hawaadhiriki na magonjwa ya milipuko hususani ugonjwa wa kipindupindu.
Zoezi hilo la usafi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam liliwahusisha Mkuu Wilaya ya Ilala, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex, wadau kutoka NMB Bank, Asasi mbalimbali ikiwemo Juza Waste Pickers Initiative, WEJISA company, Kajenjere Trading Company Limited, Satek Company, wanafunzi kutoka shule ya Sekondari ya Wavula Azania pamoja na wananchi wote wa Kata ya Ilala wakiongozwa na vijana wa usafi kutoka Machinga Complex.
Aidha Jiji la Dar es Salaam limekua na mvuto sana kutokana na kampeni hii na kwa sasa Mkoa huu ni wa mfano kwa Mikoa mingine katika kuhamasika kufanya hivi kwani hadi sasa Jiji la Dar es Salaam limeweza kushika nafasi ya sita Afrika kwa usafi wa mazingira.
“Swala la usafi ni lakwetu wote na sio la Mkuu wa Wilaya wala Mkuu wa Mkoa hivyo wote tuhakikishe tunatunza mazingira na zoezi hili la usafi ni la kudumu hivyo tutunze mazingira yetu na maeneo yetu tuyaweke katika hali ya usafi hivyo tujitokeze kwa wingi katika kushiriki usafi kwani Dar es Salaam ni miongoni mwa Mikoa tisa imago Fanya vizuri katika kupambana na ugoSnjwa wa Malaria hii yote ni kwasababu ya usafi hivyo tuhakikishe tunafyeka majani pamoja na kuzibua mitaro ili tutokomeze kabisa ugonjwa huu na tuendelee kuweka mazingira yetu katika Hali ya usafi.”
Sambamba na hilo aliongeza “Napenda kuwashukuru viongozi wa Machinga Compelex pamoja na Wafanya biashara wote kwa kujitoa katika kuhak ikisha Jiji letu linakua katika hali ya Usafi kwani kila Nikija Ilala lazima nikutane na ikiwa kampeni hii kwani wanajitoa sana kusafisha Jiji letu hivyo niwaombe wananchi na viongozi wengine kufuata mfano wa wananchi wa Machinga Complex”.
Pia Mhe. Makalla amewataka watendaji wa kata na mitaaa pamoja na Maafisa Mazingira wa Halmashauri kuhakikisha wanazunguka na kuangalia mitaa yote inakua safi huku akiwataka wafanya biashara wote kuhakikisha maeneo yote ya wazi yanaachwa kama alivyoagiza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema “Napenda kuwashukuru wadau wote wa maendeleo wanaoshirikiana nasi katika kuweka Jiji letu safi kwani jitihada zao ni kubwa sana pia nipende kutoa wito kwa viongozi wote wajitokeze kwa wingi katika kusimamia zoezi la usafi kila siku katika maeneo yao hivyo napenda kumuhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba tutasimamia zoezi hili la usafi kwa ukaribu zaidi na Ikitokea baadhi ya watu watakwamisha tutawashughulikia kwa mujibu wa Sheria.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.