• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd watoa Madawati 25 katika Shule ya Msingi Vingunguti

Posted on: March 23rd, 2023

Wafadhili kutokaTanga Pharmaceutical and Plastics Limited(TPPL) leo tarehe 23 Machi, 2023 wametoa msaada wa madawati 25 kwa Shule ya Msingi Vingunguti iliyopo Kata ya Vingunguti ikiwa ni sehemu ya mchango wa wadau wa elimu kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma katika mazingira bora na tulivu.

Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto aliwashukuru wadau hao kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu nchini huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika kujenga na kuimarisha sekta ya elimu nchini

“Halmashauri iko tayari kushirikiana na wadau wa maendeleo na nitahakikisha kuwa yote ambayo ni muhimu zaidi yatatekelezwa kwa wakati. Nawashukuru sana wadau kwa kuweza kuwa sehemu ya kuipa kipaumbele elimu Kwani Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd wamekuwa wadau wazuri sana katika kuchangia maendeleo ya Elimu katika Halmashauri yetu kwani leo hii wametoa madawati 25 kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Vingunguti huku mwaka 2020 waliweza kuchangia Friji Saba katika Kata ya Vingunguti ambazo zinasaidia katika Shule zetu na Zahanati yetu ya Vingunguti , Kwa hakika nyie ni marafiki wa kweli wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hatuwezi kuwalipa”.

Sambamba na hilo Mhe.Kumbilamoto aliweza kumkabidhi Cheti cha shukrani Meneja kutoka Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuunga mkono sekta ya elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Aidha Mhe. Kumbilamoto ametoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto wa Shule ya Msingi Vingunguti kuchangia fedha ya chakula kwa watoto wetu kwani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amekua akijitoa sana katika kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika hivyo kwa kutambua juhudi hizo wazazi wanahitaji nao kuchangia fedha kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi ili waweze kusoma kwa bidii wakiwa na afya njema.

Akikabidhi madawati kwa niaba ya wadau hao Meneja Muajiri kutoka Tanga Pharmaceutical Ltd Ndg. Stephen Godfrey amesema “Nina furaha sana kwa kampuni yetu kuwa miongoni mwa wadau wa maendeleo katika kukuza sekta ya elimu nchini hivyo nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuchochea maendeleo katika sekta ya elimu kwani juhudi zake zote ndio zimefanya leo hii sisi kuchangia madawati 25 katika shule ya Vingunguti hivyo niwaombe wanafunzi kusoma kwa bidii ili kukuza ufaulu katika Halmashauri yetu ya Jiji la Dar es Salaam.”

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Vingunguti Mwl. Mfaume Fadhili amesema “Tunaishukuru sana kampuni ya Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd kwa kuwa mdau wetu mzuri wa maendeleo katika kukuza sekta ya elimu kwani hii leo tunafuraha kupata madawati haya 25 ambapo kwa kiwango chake tumendelea kupunguza idadi ya uhitaji wa madawati katika shule hii ya Msingi Vingunguti yenye jumla ya wanafunzi 2514. Pia tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka hii miwili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu kwani tuliweza kupata madawati 50."

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.