• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Uzinduzi wa mafunzo ya mfumo mpya wa Mipango na Bajeti wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

Posted on: July 24th, 2017

Mafunzo ya mfumo mpya wa Mipango na Bajeti (Planrep) yamezinduliwa leo Mkoani Mtwara kwa Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya, Maafisa TEHAMA, Maafisa  Mipango, Wahasibu,  na Wachumi kutoka katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Dar es Salaam.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Elias Nyabusami amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na yatasaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani zikiwemo uwepo wa matoleo tofauti tofauti ya mfumo wa mipango na bajeti gharama kubwa zilizotumika pamoja na muda mrefu uliokuwa unatumika wakati wa kuandaa bajeti.

Akifafanua amesema kuwa mfumo huo mpya toleo la mtandao “Web based” utasaidia kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa ngazi husika za utawala kwa wakati na hakutakuwa tena na haja ya wahusika kusafiri  kutoka katika vituo vyao vya kazi ili kushughulikia masuala ya Bajeti na Mipango kwa kuwa sasa yatafanyika katika Mikoa na Halmashauri husika na taarifa hizo kupatikana katika ngazi mbalimbali kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Kwa upande wake Mkuu wa timu ya Rasilimali Fedha Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama “Public Sector Systems Streghthen (PS3)”  Bw. Germini Mtei amesema kuwa kupitia mfumo mpya wa PlanRep Mipango yote na Bajeti za Vituo vya kutolea Huduma kwa wananchi itaonekana kupitia mfumo huo hali itakayosaidia kuongeza ufanisi, uwazi, uwajibikaji na kuboreshwa kwa utoaji huduma.

“Kwa kutumia mfumo huu mpya sasa tunaamini kuwa utasaidia kuondoa ucheleweshaji wa fedha kwenda kwenye miradi na upotevu wa fedha kwa kuwa kila kitu kitafanyika kwa njia ya mtandao” Alisisitiza Bw.Mtei.

Aliongeza kuwa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani “USAID” ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara katika maeneo yafuatayo:-

  1. Utawala bora na ushirikishwaji wa raia
  2. Raslimali watu
  3. Raslimali fedha
  4. Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
  5. Tafiti tendaji

Aidha Afisa TEHAMA Mwandamizi toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Archibold Kundasai amesema kuwa mipango yote kuanzia ngazi ya Kata, Halmashauri na Mikoa itakuwa katika mfumo huo na dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia Wananchi kwa kuhakikisha kwamba mifumo yote ya TEHAMA inazungumza ili kubadilishana taarifa.

“Bajeti ilikuwa ikichukua muda mrefu kuandaliwa ambapo takribani miezi 4 ilitumika ambapo kwa mfumo huu tija itaongezeka kwa kuwa wahusika watabaki katika vituo vyao wakihudumia wananchi huku wakitekeleza jukumu la kuandaa Bajeti na Mipango yao” Alisisitiza Kundasai.

Serikali ya Tanzania na USAID kupitia mradi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) imeandaa mafunzo haya kwa watumiaji wake nchi nzima. Mafunzo yanatolewa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wakala ya Serikali mtandao, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Afya na unatarajiwa kutumiwa na watumiaji 1,500 watakaofundishwa matumizi ya mfumo huo.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.