Na; Judith Msuya
Mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo August 25, 2021 wamezindua mradi wa ukarabati wa miundombinu ya maji safi na salama pamoja na uwekaji wa tank la liter Laki 1 katika ukumbi wa Gereza la Maabusu Segerea lengo likiwa ni kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika Gereza hilo.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mratibu wa TASAF - Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Bi. Marcella Msawangwa amesema kuwa mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) kwa awamu ya Tatu ambao ulizinduliwa kwa lengo la kunusuru kaya maskini katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na kusaidia jamii kutekeleza miundombinu ya Maji na barabara ameona kuwa hanabudi I us a id is upatikaji wa maji safi na salama kwa Gereza la Maabusu Segerea ili kuweza kutatua changamoto ya maji katika Gereza hilo.
Aidha Bi. Maricella ameeleza kuwa mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika Desemba, 2021 utagharimu takribani shillingi million 197 ambapo mradi huo utaanza kutekelezwa mara baada ya mafunzo ya siku tatu (3) ambayo yalizinduliwa katika hafla na kuanza rasmi Agust 25 hadi Agust 27, 2021 hivyo baada ya mafunzo hayo kukamilika mradi utaanza kutekelezwa kwani utaratibu wa manunuzi pamoja na kupata local fundi ushaanza kufanyika.
"Ni matumaini yangu kuwa kwakua tushatangaza tender za kupata local fundi mara baada ya mafunzo tutaanza utekelezaji wa mradi ambao unatarajiwa kukamilika Desember 2021 kwani fedha ya kutosha ipo hivyo hakutakua na changamoto ya kifedha itayokwamisha mradi huu".alieleza Bi.Marcella.
Vilevile, Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Gereza la Maabusu Sagerea Mrakibu wa Maabusu Athanas Ndowano ameeleza kuwa tatizo la maji katika Gereza hilo ni kubwa ukilinganisha na mahitaji ya watu waliopo maabusu hivyo ujio wa mradi huu ni ukumbozi mkubwa kwa Gereza la Maabusu Segerea pamoja na wananchi wa mtaa wa Mgombani na Kata za jirani ambao wataweza kufaidika na mradi huu.
"Tatizo la maji lilikua kubwa hivyo tunatoa shukrani zetu kwa Mradi wa maendeleo ya Jamii (TASAF) pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona tatizo la Magereza kama sehemu yao hivyo tunaahidi kufanya kazi kwa uweledi mkubwa kama ilivyokusudiwa".alisema Mkaribu Athanas.
Sambamba na hilo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam Comisioner msaidizi wa Magereza Focus Ndabita ameahidi kuwa watasimamia kamati ya ujenzi wa mradi huo na watahakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na weledi mkubwa ili ujenzi huo uweze kukamilika kwa wakati.
Akifungua mafunzo pamoja na kuzindua mradi huo wa ukarabati wa miundombinu ya maji safi na salama pamoja na ujenzi wa tank la lita Laki 1 kwa niaba ya Mkurugunzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Rajabu Ngoda amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa mradi huo pamoja na utunzaji wa nyaraka ili hata ifikapo kipindi cha Mwenge wa Uhuru 2022 mradi uweze kuwekewa jiwe la Msingi bila dosari yoyote.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.