Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ametenga zaidi ya shilingi Bilioni 11 Kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi katika kujikwamua Kiuchumi.
Mhe. Mpogolo ameyabainisha hayo leo Oktoba 23, 2024 Jijini Dar es salaam mara baada ya kufunga Mafunzo yyaliofanyika muda wa siku tatu kwa Wajasiriamali 600 katika Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE yalioenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya chuo hicho.
Amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha Wana Ilala wanajikwamua kiuchumi na kuliwezesha Taifa kupata Maendeleo hivyo Serikali imeamua kuwa na makundi matatu ya utoaji mikopo ambapo kundi la kwanza litapewa kuanzia shilingi laki 5 hadi milioni 10 la pili milioni 10 hadi 50 na la tatu milioni 50 hadi 150.
"Sisi kama Jiji tunakwenda kulipa kipaumbele kundi la kwanza kwasababu ndio lenye kina Mama wengi ambao wanakabiliwa na changamoto ya masuala ya mikopo ya kausha damu hivyo tunakwenda kutatua changamoto hii." Ameema Mpogolo.
Amesema ni tija kwa Wafanyabiashara kupata Elimu hio katika kufanya Biashara zao hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuirejesha mikopo ya asilimia 10.
Katika kumuunga mkono Rais Samia kwenye kuhakikisha Nchi inaacha matumizi ya nishati chafu badala yake inatumia nishati safi, Jiji limejipanga kuwakopesha majiko ya Gesi Mama Lishe na Baba ili waweze kuokoa kiasi Cha pesa shilingi elfu 40 hadi 50 kwa wiki.
"Sambamba na hayo tunakwenda kuwasaidia Vijana wa bodaboda zaidi ya 150,000 Kwa kuwapa Elimu ya kibiashara,Usalama Barabarani na Elimu ya mikopo." Ameongeza Mhe. Mpogolo.
Nae Mkuu wa Chuo Cha CBE Prof. Edda Tandi Lwoga amesema watahakikisha Elimu hio walioitoa Kwa Wajasiriamali hao inakwenda kuenea Nchi nzima ili Watanzania waweze kuwa na uelewa juu ya masuala ya Mikopo na Biashara.
Nao Baadhi ya Wajasiriamali walioshiriki Mafunzo hayo wameishukuru Serikali Kwa kuwapa fursa hio ambapo Mafunzo hayo yamewafungua katika kuwawezesha kibiashara na kuiomba Serikali iendelee kuawatafuta kwani wengi wao hawana Elimu ya Biashara.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.