Na: Doina Mwambagi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, amewataka viongozi na watendaji wa Halmashauri nchini kuhakikisha hawawafumbii macho wakandarasi wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Ameyasema hayo leo Mei 24, 2025 katika hafla ya uzinduzi wa soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto, lililopo kata ya Vingunguti jijini dar es salaam.
Waziri Mchengerwa amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati, hivyo ni muhimu wakandarasi wote waliopata zabuni kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa.
“Tunataka kuona barabara zinajengwa kwa viwango na kwa wakati, hatuwezi kuendelea kuvumilia wakandarasi wazembe wanaokwamisha juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo." Alisema Mchengerwa.
Sambamba na hilo, Waziri Mchengerwa ameipongeza halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa hatua nzuri ya kurekebisha miundombinu ya barabara, akisema kuwa juhudi hizo zimekuwa msaada mkubwa katika kuwaunganisha wananchi kutoka sehemu moja hadi nyingine, na kukuza biashara katika maeneo mbalimbali ya Jiji hili.
Katika hatua nyingine, Waziri mchengerwa ameshuhudia utiaji saini wa mikataba sita ya ujenzi wa barabara , madaraja na uboreshwaji wa jengo la mkutano Anatouglo.
Soko hilo la kisasa la Kumbilamoto lenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 230 litakuwa suluhisho kwa wafanyabiashara hao ambao hapo awali walikuwa wakifanya biashara zao katika mazingira ambayo hayakuwa rafiki.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.