Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo waliosajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NINs) kwenda kuchukua vitambulisho vyao kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa ili kuepukana na changamoto zitakozojitokeza Baada ya Kupitia Kwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo. Mhe. Chalamila ameyasema leo Desemba 22, 2023 wakati wa zoezi la kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa Kata ya Vingunguti uliofanyika kwenye viwanja vya Msikate Tamaa.
”Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwa kuongeza kasi ya utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa, hivyo niwaombe wananchi kufuata vitambulisho ili gharama za utengenezaji zilizotumika zisiende bure. Kitambulisho kinafaida kubwa sana katika kukutambulisha mwananchi kuliko namba.
Pia natoa pole kwa wananchi wote wa Kata ya Vingunguti kwa athari za mvua mlizokutana nazo na niwahakikishie tutarekebisha miundombinu yote ya barabara na vivuko vilivyoharibika." Amesema Mhe. Chalamila.
Aidha, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Diwani wa Kata ya Vingunguti Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa kwa kufika katika Kata yake na kuongea na wananchi na kumuahidi kushirikiana nae pale atakapomuhitaji.
Zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Mkoa wa Dar es Salaam lilianza Tarehe 12 Desemba, 2023 na litadumu kwa siku kumi na nne (14).
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.