Wananchi Wilayani Ilala, Mkoani Dar es Salaam, wameungana na Watanzania katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano, huku Mkuu wa Wilaya Mhe. Edward Mpogolo akitoa wito wa kuendelea kuuenzi, kuutunza na kuutetea Muungano.
Akihutubia wananchi, viongozi na wadau waliojitokeza kufanya usafi wa mazingira katika soko la samaki feri, jijini Dar es Salaam, Mhe. Mpogolo amesema dhamana ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iko kwa kila Mtanzania.
Ameeleza kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliotimiza miaka 61 ni kielelezo cha Tunu ya Taifa iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shekhe Abed Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
Mhe. Mpogolo amebainisha katika soko la samaki feri, yalilofanyika maadhimishisho ya mika 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sehemu ambayo inadhihirisha Muungano uliopo kwa watanzania wanaofanya biashara katika soko ilo kuwa na muingiliano wa makabila na tabaka tofauti toka upande wa bara na visiwani.
Ameongeza kuwa kaulimbiu ya Miaka 61 ya Muungano, imebeba dhima ya kuchagua viongozi bora kwa kufanyika uchaguzi kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa katiba kumchagua Rais wa Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye anajukumu la kuunda serikali na kutunza Tunu ya Muungano.
Kuhusu suala la Ushiriki wa Uchaguzi Mkuu, Mhe. Mpogolo, amewahimiza wananchi wenye sifa kushiriki zoezi ilo na kuchagua viongozi bora pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano kwa taifa.
Aidha, Maadhimisho hayo ya Muungano, kwa wilaya ya Ilala yaliyoadhimishwa kwa kufanya usafi soko la samaki feri, upandaji miti katika msitu wa zingiziwa, na usafishaji eneo la fukwe za bahari ya Hindi kwa kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Ilala, Mkoani Dar es salaam Elihuruma Mabelya ametumia nafasi hiyo kuwahimiza vijana kuwa wazalendo na kudumisha Muungano ili uendelee kuwa wa mfano.
Nae, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar licha ya kuwa wa nchi moja bali umejenga udugu, ujamaa na kuondoa kero zilizokuwa miaka ya nyuma ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.