Katika kutegeleza Agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango kuwa ndani ya siku 90 Halmashauri zihakikishe zinatambua Day Care zote zilizokidhi vigezo vya ubora na ambazo hazijakidhi vigezo zifungiwe, hivyo katika kutekeleza agizo hilo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Afya divisheni ya Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala leo Septemba 12, 2023 wameandaa mafunzo kwa walezi na wamiliki wa Day Care yenye lengo la kuwapa elimu kuhusu maswala ya lishe, Ustawi wa jamii na afya kwa ajili ya makuzi ya watoto mashuleni ikiwa ninsehemu ya kutekeleza Ilani kama inavyoagiza.
Aidha, Katibu wazazi wilaya ya Ilala Mhe. Mtiti Mbassa Jirabi ameeleza kuwa “Jumuiya hii ni chombo kinachoongozwa na Chama cha Mapinduzi yenye majukumu ya kueleza kufafanua na kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa sera ya malezi kwa watoto na vijana wa Tanzania pamoja na kujishughulisha na maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla kama inavyoelezwa katika kitabu cha ilani kifungu 4 uk (iii) hivyo katika kutekeleza ilani tumefanya mafunzo haya ili kujua ufanisi wa malezi ya watoto katika vituo hivyi na kuhakikisha utekelezaji wa sera ya malezi kwa watoto pia tukitaka kujua changamoto zinazowakabili walezi na wamiliki wa Day Care hizi hivyo niwaombe Maafisa Ustawi kuhakikisha tunashikamana na kuwafundisha watoto wetu ili waweze kukua katika utamaduni wa Taifa letu.”
Akiongea katika mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Zeituni Hamza ameeleza uwepo wa maji safi katika vituo, uwepo wa vyoo safi na salama na usafi wa mazingira na mtu binafsi katika vituo vya kulelea watoto ili kuepukana na magonjwa kwani mazingira bora ni dhana bora katika kuwajengea watoto uwezo wa kufikiri na kupata malezi bora.
"Mmepewa dhamana na jukumu kubwa la kukaa na watoto wanapokuwa mashuleni hakikisheni mazingira yana kuwa safi na salama japo ulezi sio kitu rahisi sana lakini tuhakikishe tunaitunza dhima ya nchi yetu kuhakikisha watoto wetu wanapata afya na elimu bora."
Kwa upande wake mratibu wa malezi ya watoto Wilaya ya Ilala Bi. Suzan Mdesaameeleza maswala yambalimbali ya usalama kwa watoto ikiwemo Day care zote kuzungushiwa ukuta ila kuepukana na ukatili wa kijinsia kwa watoto mashuleni kwa hivyo amewaasa walezi na wasimamizi wa shule kuhakikisha wanazingatia malezi ya watoto hao sambamba na kuhakikisha wazazi wanazingatia kuzungumza na watoto mara kwa mara ili kujua endapo kuna changamoto zinazowakabili.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.