• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Wananchi Wahamasishwa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia

Posted on: September 27th, 2024

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira anayeshughulikia masuala ya Mazingira Bi.Christina Mndeme ametoa wito kwa mama lishe na Baba lishe  kuokoa maisha yao kwa  kutumia nishati safi ya kupikia ambayo itawaepusha na athari katika mfumo wa upumuaji pamoja na utunzaji  wa mazingira.

Bi.Mndeme ameyasema hayo leo, Septemba 27, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya ugawaji wa majiko ya kupikia kwa mama na baba lishe wa Kisutu iliyoandaliwa na Kampuni ya Bakhresa yenye lengo la  kuunga mkono jitihada za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza katika hafla hiyo Bi. Mndeme amesema, Rais Samia licha ya kuwa kinara wa Afrika kwenye kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, pia amedhamiria kuwaondoa kina mama na baba lishe wa Tanzania katika matumizi ya nishati isiyo safi na pia kuboresha hali zao kwa kutumia nishati safi ya kupikia ambapo hii inaendana na kampeni ya kumtua mama kuni kichwani.

‘‘Nipende kupongeza sana Makampuni ya Bakhera kwa kuibeba ajenda hii ya nishati safi ya kupikia kwani mmeonesha kwa vitendo kuhakikisha mnamuunga mkono Rais wetu katika kuhakikisha tunatunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia ambayo itaepusha athari zote za kimazingira zitokanazo na matumizi ya nishati isiyo safi, hivyo nitoe wito kwa wadau wengine kuhakikisha wanashirikiana na sisi katika kutunza mazingira ili hadi kufikia mwaka 2034 asilimia 80% ya watu wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia."

Sambamba na hilo, Bi. Mndeme ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa ujumla itaondoa uharibifu wa mazingira ambapo jamii itaachana na ukataji wa miti ovyo pamoja na kumtua mama kuni kichwani kwa kuwauondolea wanawake kutumia muda  mwingi katika kutafuta kuni badala yake kufanya shughuli za Kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Theresia Denis ameishukuru Kampuni ya Bakhressa kwa kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akieleza kuwa Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanatimia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na athari za kimazingira na kuendelea kulinda mazingira na afya kwa ujumla.

Naye Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Makampuni ya Bakhressa Bi. Rehema Salim ameeleza kuwa katika kurudiasha fadhila kwa jamii Kampuni ya Bakhresa imeona ni vyema kuunga mkono  juhudi za Mheshimiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani za matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo wameanza kwa kugawa majiko 60 kwa mama lishe na baba lishe wa Kisutu huku akieleza kuwa kampeni hii ni endelevu na itafanyika nchi nzima.

Aidha, mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ulizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Mei 8, 2024 ukilenga kuepuka athari za matumizi ya kuni na mkaa unaoambatana na utunzaji wa mazingira.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.