• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Wasimamizi wa Uchaguzi Jiji la DSM watakiwa kufuata maelekezo na sio kufanya kazi kwa mazoea

Posted on: October 1st, 2024

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kufuata maelekezo na sio kufanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na kanuni ili kuepusha sintofahamu zinazoweza kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024 Sambamba na kauli mbiu isemayo "Serikali za Mitaa sauti ya Wananchi jitokeze kushiriki Uchaguzi".

Wito huo umetolewa leo Oktoba Mosi, 2024 wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi kwa ngazi ya Jimbo, Kata na Mtaa uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam .

Aidha, Ndg. Mabelya ameeleza kuwa mafunzo hayo ya siku (1) yamelenga kuhakikisha kwamba uchaguzi unafanyika kwa haki na ufanisi, huku yakiwaandaa wasimamizi wasaidizi na kuwapa ujuzi wa kutosha katika kusimamia mchakato wa uchaguzi kwa kuhakikisha kwamba kila hatua inatekelezwa kwa mujibu wa sheria, Kanuni na taratibu za uchaguzi.

"Kwa mamlaka niliyopewa na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kifungu cha 201A cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) sura 288 kifungu cha 57(3) cha Sheria za Serikali za Mitaa pamoja na kanuni ya 7(1) ya uchaguzi wa viongozi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa 2024 zilizotolewa kwa tangazo la Serikali namba 571,574 na 575 ya mwaka 2024 na Mwongozo wa Uchaguzi wa tarehe 09, Septemba  2024 vilivyotumika kwa ajili ya kuwateuwa kuwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo naamini baada ya mafunzo haya uchaguzi utafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi ili kuondoa malalamiko wakati wote wa uchaguzi."

Sambamba na hilo, Ndg.Mabelya amewataka washiriki hao kuzingatia mafunzo pamoja na kutoa uzoefu wao wa usimamizi wa siku za nyuma ili iwe rahisi katika utekelezaji wa jukumu zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27, 2024 huku akiwakumbusha kuzingatia falsafa ya 4R (Reconciliation, Reform, Resilience na Rebuild) ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kifanikisha zoezi hilo kwa haki na uzalendo kwa maslahi ya Jiji na Nchi kwa ujumla.

Halikadhalika, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wamekula kiapo cha uaminifu, utii ,uadilifu na kutunza siri  katika kutimiza majukumu yao na kuwatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.





Announcements

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2025 July 08, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA February 28, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • Mkurugenzi Mabelya ajifungia na watendaji wake kwa siku 2 kuweka mikakati ya ukusanyaji mapato

    July 17, 2025
  • "Tanzania ina umeme wa kutosha" - Mhe. Dkt. Biteko

    July 11, 2025
  • Jiji la Chengdu China kuanzisha uhusiano wa ushirikiano na Jiji la Dar es Salaam

    July 08, 2025
  • Mikopo ya asilimia 10 imekuza mitaji ya wajasiriamali wadogo - DC Mpogolo

    July 07, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.