• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Watahiniwa 21440 Jiji la Dar es Salaam watarajiwa kumaliza kidato cha nne

Posted on: November 14th, 2022

Watahiniwa wapatao 21440,katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Tarehe 14 Novemba,2022 wameungana na maelfu ya watahiniwa wengine kote nchini kuanza kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne.

Akitoa taarifa juu ya watahiniwa hao Mwl.Musa Ally ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amesema kuwa wao kama walimu wamejiandaa vizuri katika kuwaandaa watahiniwa wao na wana matarajio makubwa juu yao kuwa watafanya vizuri kama ilivyo ada.

Aidha Mwl. Musa ametoa mchanganuo wa takwimu za watahiniwa hao na kusema kuwa katika watahiniwa 21440, wavulana ni 10969 na wasichana ni 10471. Pia kuna watahiniwa wa mitihani ya maarifa maarufu kama QT na wale wa mitihani ya kidato cha nne, ambapo watahiniwa wa mtihani wa Maarifa  wapo 9971,watahiniwa wa kujitegemea ni 2164 na watahiniwa wa shuleni ni 18305.

Kwa upande wa watahiniwa walio na mahitaji maalum,amesema kuwa kuna jumla ya watahiniwa 43, ambapo 17 wapo katika shule ya Sekondari Jangwani, 25 wapo Pugu Sekondari  na 1 yupo katika shule ya Sekondari Alhalamain.

Ameongeza kuwa watahiniwa hao wote wapo katika vituo 101 vya shuleni na vituo 8 vya watahiniwa wa kujitegemea.

Sambamba na Takwimu hizo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha sekta ya elimu nchini na kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama ya Watoto kujifunzia.

“Ninamshukuru Mhe.Rais kwa namna anavyoendelea kuiwezesha sekta ya elimu kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, ambapo wamekuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali  na kuboresha miundombinu ya kutolea elimu nchini.” Amesema Mwl.Musa.

Akiongea kwa niaba ya wakuu wote wa shule za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mwl.Joseph Deo ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini W.Mkapa amesema kuwa wao Kama Walimu wamewaandaa vizuri watoto hao sio tu kwa elimu ya darasani bali ya maisha pia,hivyo wana matarajio makubwa kuwa watafanya vizuri na ufaulu wao utakuwa wa juu kuliko mwaka uliopita.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.