Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam waelekezwa kuhakikisha wanawajibika na wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia taratibu za utendaji kazi, sheria, kanuni na miongozo iliyopo.
Hayo yamebainishwa leo Machi 03,2023 wakati wa Kikao kazi na Maafisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Wahasibu wanaokusanya mapato, Watendaji wa Kata, Auxiliary Polisi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Watumishi wengine kutoka idara ya ya Utumishi na Idara ya Uwekezaji, viwanda na biashara kilichofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kujadili na kuweka mikakati madhubuti juu ya ukusanyaji wa mapato yanayokusanywa kwenye vyanzo mbalimbali vyaHalmashauri ya Jiji.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Afisa Utumishi wa Jiji hilo Bi. Susan Mahhu ameeleza kuwa baada ya vikao vya Bajeti kufanyika na kupitiwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweza kuongezewa kiasi cha ukusanyaji wa mapato kwa Asilimia 35 kutoka kukusanya bilioni 81 hadi Bilioni 102 hivyo kikao hiki kimefanyika kwa lengo la kuwakumbusha watumishi kutekeleza majukumu yao na kwa kasi zaidi ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali.
Aidha Bi. Susan ameendelea kusema “Watumishi wengi wanaonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kutokuwajibika kwani wengi imeonekana kutokufika kwenye maeneo yaonya kazi kwa wakati. Pia Wafanyabiashara wengi wameonekana kulalamikia polisi hivyo niwaombe Polisi tutekeleze majukumu yetu kwa haki na usawa tusimpendelee wala kumuona mtu yoyote vilevile nawakumbusha muwahi katika vituo vya kazi lengo letu ni kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha hali ya juu.”
Sambamba na hilo amewataka watumishi wote wanaofanya kazi kwenye Kata wafike kazini kwa wakati na kutakua na mahudhurio katika Kata na ikitokea mtu hawajibiki atawajibishwa kwa kufuata sheria na Kanuni za utendaji kazi.
Naye Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Nickas Msemwa amesema “Nipende kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kufanya kikao hiki kwani kupitia kikao hiki naamini kila mmoja ataenda kutekeleza majukumu yake ipasavyo pia kwa upande wetu maafisa biashara tuhakikishe tunawajibika ipasavyo kwani Bajeti imeongezeka kwa asilimia 35% kutoka bilioni 81 hadi bilioni 102 tofauti na ilivyokua awali hivyo Utendaji wa kazi unatakiwa ubadilike kuendana na jukumu kuongezeka, hivyo tunatakiwa tufanye kazi kwa ushirikiano na tuweke mikakati mathubuti kwenye vyanzo vyetu na pia kila mtu abadilike na awajibike katika eneo lake.
Pia ameendelea kusema mikakati hiyo itaanzaia katika kata na kila Kata wajiwekee malengo katika ukusanyaji wa mapato na endapo Kata itakusanya zaidi ya malengo fedha hizo zinaweza kutumika katika kutatua changamoto za Kata hizo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.