Katika kuhakikisha Halmashauri Jiji la Dar es Salaam inaendelea kuboresha utoaji wa huduma bora wa wananchi, Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wanaohudumu Kanda Namba 3 inayojumuisha Kata za Vingunguti, Kipawa, Buguruni, Mnyamani, Kiwalani na Minazi Mirefu, leo tarehe 23 Oktoba, 2023 wamefanya ziara ya mafunzo kwenye Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili kujifunza katika maeneo ya kutolea huduma pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Akiongea wakati wa Mafunzo hayo Meneja wa Kanda namba 3 Bw. Kefa Dan Gembe ameeleza kuwa lengo la ziara hii ni kujifunza namna gani Halmashauri nyingine zinafanya kazi katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na maeneo mengine ya kiutendaji.
"Lengo la ziara hii ni kujifunza kutoka kwa Halmashauri nyingine namna gani wanafanya kazi katika vyanzo vyao vya mapato walivyonavyo hivyo tutafanya ziara hapa Jiji la Dodoma kwa siku moja na kisha Jiji la Arusha ambapo baada ya ziara hii tutakuja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha Jiji latu linafanya vizuri katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo."
Vilevile Bw. Kefa Ameendelea kusema “Matarajio yetu baada ya ziara hii ni kuongeza ufanisi katika maeneo ya usimamizi wa usafi, kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato, na usimamizi wa miradi kwani dhana ya Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kufanya kazi kwa ubunifu na ufanisi wa hali ya juu bila kusahau kuwahudumia wananchi wetu kwa wakati na kwa ukaribu zaidi."
Itakumbukwa kuwa lengo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzisha kanda ni kurahisisha utoaji wa huduma unaolenga kutoa huduma zenye ubora na usawa kwa jamii kwa kuzingatia utawala bora na kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.