Afisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Frola Mgonja amesema mahusiano mazuri kati ya wazazi, walezi na watoto ni muhimu katika makuzi ya watoto kwani husaidia kubaini vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto.
Bi. Flora ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala alipokua akiongea na watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika ukumbi wa Shule ya Msingi Kisutu kwenye Tamasha la Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kata ya Kisutu yenye kaulimbiu “WEKEZA: KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA”.
Sambamba na hilo, Bi Flora amesema “Watoto wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa ili waweze kutimiza ndoto zao na Serikali inapinga ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa kuhakikisha tunawalinda na kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu. Serikali kwa kupitia wadau mbalimbali tutahakikisha na kusimamia watoto wote wanaoishi kwenye mazingira magumu kuwapatia ajira zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi”
Aidha, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Ilala Mititi Mbasa amewashukuru Ustawi wa Jamii Kata ya Kisutu kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuahidi kushirikiana nao kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi yaliyo mema.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata ya Kisutu Bi. Joyce Maketa amesema “Watoto wa mtaani wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa chakula, mavazi, pia wamekua wakifanyiwa ukatili ikiwepo kupigwa, kubakwa na kulawitiwa, hivyo wanaomba Serikali kuwapatia makazi ya kuishi na ajira ili waepukane na changamoto zinazowakabili."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.