Na: Hashim Jumbe, Mkoani Tabora
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo tarehe 04 Agosti, 2022 amefungua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa ngazi ya Kitaifa, kwa mwaka 2022 ufunguzi uliofanyika kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi uliopo Mkoani Tabora.
Mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi tangu tarehe 29 Julai, 2022 na yanatarajiwa kufungwa tarehe 19 Agosti, 2022 ambapo yanajumuisha timu kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara na Mikoa ya Pemba na Unguja na Jumla ya wanamichezo 3,274 wanashiriki UMITASHUMTA na kwa upande wa UMISSETA Jumla yao itakuwa ni wanamichezo 3,497
Aidha, wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewaasa wanamichezo hao kucheza kwa bidii kwani michezo inatoa fursa mbalimbali
"Ndugu wanamichezo, matarajio ya Viongozi wetu yanatokana na ukweli kuwa wanamichezo wanaweza kuimarika na kuwa bora katika kupata fursa ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ikiwemo mashindano haya ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA na kwa mantiki hiyo Serikali zetu zote Mbili (2) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar zitaendelea kuhakikisha kwamba tunaimarisha michezo nchini kwenye ngazi zetu za shule za Msingi na Sekondari, lakini pia haitoshi Sekondari peke yake, itaenda katika vyuo vya elimu ya juu" Mhe. Majaliwa
Aidha, michezo itakayoshindaniwa kuwa ni Mpira wa Miguu Wavulana na Wasichana, Mpira wa Miguu Maalum (Wavulana viziwi) Netiboli kwa Wasichana, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kengele kwa Wasioona, Riadha Maalum, Riadha kawaida naSanaa za Maonesho.
Sambamba na michezo hiyo, lakini pia kutakuwa na Mpira wa Kikapu utakaohusisha wanafunzi wa Sekondari Wavulana na Wasichana, hivyo kufanya UMISSETA kuwa na Jumla ya Michezo Kumi (10) na UMITASHUMTA michezo Tisa (9)
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanafanyika Mkoani Tabora ikiwa imepita miaka 22 tangu mara ya mwisho kufanyika Mkoani hapa, hivyo kwa mwaka huu michezo inaendelea kufanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Tabora, Shule ya Sekondari Tabora Boys na Tabora Girls na Chuo cha Uhazili Tabora
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.