Katibu Tawala wa Wilaya ya Wilaya Bi. Charangwa Selemani leo tarehe 3 Agosti, 2023 amefungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani katika Kituo cha Afya Chanjka kwa lengo la kuelimisha na kutambua umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Bi. Charangwa amesema kuwa uzinduzi wa Wiki ya Unyonyeshaji ya Maziwa ya Mama kwa mtoto una lengo la kuongeza wigo wa uelewa na kuwakumbusha kina mama na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa kunyonyesha.
“Leo tumekuja kufungua maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji katika Kituo hiki cha Afya ikiwa moja ya Wiki ambayo inatambulika Kitaifa na Duniani kote na lengo kubwa likiwa nikuongeza uelewa na kuelimishana juu ya umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto. Pamoja na hilo, elimu itatolewa kwenye Vituo vyote vya Afya hivyo niwasihi akina mama wote wenye ujazito na wenye watoto wenye umri chini ya miaka kuhudhuria.” Amesema Bi. Charangwa.
Nae Mganga Mkuu wa Jiji la DSM Dkt. Zaituni Hamza amewaasa akina mama wenye watoto kufuata taratibu za unyonyeshaji kama zilivyooneshwa na wataalamu na kuhakikisha wanapata mlo kamili ili waweze kuzalisha maziwa kwa wingi kwaajili ya watoto wao.
“Akina mama wenzangu wenye watoto naomba mfuate taratibu zote za unyonyeshaji na kuacha dhana potofu zinazozongumzwa na watu kama vile kumlisha mtoto chakula kizito kama uji ilihali muda bado." Amesema Dkt. Zaituni
Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji 2023 yenye kauli mbiu isemayo "Saidia Unyonyeshaji: Wezesha wazazi kulea watoto na kufanya kazi zao kila siku” yalianza tarehe 1 Agosti, 2023 na yatafikia kilele tarehe 8 Agosti, 2023.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.