Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles leo tarehe 28 Mei, 2019 akiongozana na Waheshimiwa Madiwani na Wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua maeneo ya miradi ya maendeleo ya Shirika la Masoko Kariakoo.
Maeneo ya Shirika yaliyotembelewa ni viwanja katika mitaa ya Tabata na Mbezi Beach Makonde ambayo Shirika la Masoko Kariakoo limepanga kufanya uwekezaji wa ujenzi wa Masoko ya Kisasa kwa lengo kutoa huduma nzuri na endelevu hususani mazao ya vyakula, pembejeo za kilimo na bidhaa mchanganyiko zenye kujali afya, mazingira na usalama wa watumiaji/walaji.
Waheshimiwa Madiwani baada ya kujionea hali halisi ya maeneo ya uwekezaji walipata fursa ya kutoa michango yao kwa Menejimenti ya Shirika juu ya uendelezaji na uwekezaji wa maeneo husika ikiwa ni pamoja na kujenga masoko mengine mapya katika Jiji la Dar es Salaam na kusimamia uendeshaji wake ikiwa ni sehemu mojawapo ya majukumu mahsusi ya Shirika la Masoko Kariakoo.
Shirika la Masoko Kariakoo lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge Na.36 ya mwaka 1974. Mnamo mwaka 1985, sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho kwa kurekebisha kifungu Namba 8 cha sheria hiyo. Katika marekebisho hayo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lilimilikishwa asilimia 51 ya hisa na Msajili wa Hazina akabaki na hisa asilimia 49.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.