Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles akiwa na wajumbe wa Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na timu ya Menejimenti wamefanya ziara ya kukagua mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuboresha maeneo ya fukwe katika Jiji la Dar es Salaam.
Mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuboresha maeneo ya fukwe kwa lengo la kuzuia mmomonyoko ni jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuzuia mmomonyoko wa udongo katika kingo za bahari ya Hindi katika maeneo ya barabara ya Barack Obama (Ocean Road) na Chuo cha Mwalimu Nyerere kwa upande wa Kigamboni.
Mradi wa huu wa kuta za mita 820 katika fukwe za bahari na mifereji ya maji unatekelezwa kupitia Programu ya Umoja wa Mataifa inaloshughulika na Mazingira “United Nations Environmental Programme” chini ya “United Nations Office for Project Services, Nairobi Operational Hub” na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mradi huu unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2017 utazikinga kingo za bahari na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na:
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.