Wednesday 22nd, January 2025
@Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Kila tarehe 5 Juni, kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliamuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira huko Stockholm, nchini Sweden.
Aidha, Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani United Nations Environment Programme (UNEP) lilipitishwa pia siku hiyo. Tangu wakati huo, nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kila mwaka tarehe 5 Juni, kwa ujumbe maalumu unaotolewa na Umoja wa Mataifa.
Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira. Aidha, tunatumia siku hii kutoa fursa kwa jamii kufahamu kwamba wao wana wajibu wa kuzuia madhara na mabadiliko hasi katika Mazingira na kuhamasisha jamii kufanya mazingira yao kuwa salama na masafi katika maisha yetu na vizazi vyetu.
Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho haya kimataifa ni “Connecting People to Nature”. Kwa Kiswahili ni: “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira”. Kauli mbiu hii inahamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia yetu na kuhamasishana kuyatunza na kuhifadhi.
Pamoja na kauli mbiu ya kimataifa, kauli mbiu yetu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira mwaka huu kitaifa ni "Hifadhi ya Mazingira: Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.”
Maadhimisho haya kimkoa yatafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita na nusu za mchana.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.