• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

DC Ilala azindua zoezi la Upimaji Afya bure kwa Wakazi wa Wilaya ya Ilala

Tarehe iliyowekwa: June 11th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ngw'ilabuzu Ludigija leo Juni 11 amezindua zoezi la Upimaji Afya Bure ambalo litafanyika kwa muda wa siku mbili kaanzia Leo tarehe 11 hadi 12 Juni 2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo Wakazi wakazi  wa Wilaya ya Ilala  watapata Fursa ya kupima magonjwa Bure Chini ya madaktari bingwa na wabobezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam  mheshimiwa Ludigija  amesema lengo la Kampeni ni kuwafikia wananchi wengi zaidi wa Wilaya ya Ilala kwani nifursa pekee kwa wananchi wasio na bima za afya, watoto yatima pamoja  na wananchi wote wasio na uwezo wataweza kuhudumiwa bure lengo likiwa nikuhakikisha afya za Watanzania zinakua imara zaidi.

Hata hivyo mheshimiwa Ludigija amesema" katika zoezi hili madaktari bingwa kutoka Hospital mbalimbali watahudumu zikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Taasisi ya mifupa MOI, Hospital ya Taifa Muhimbili, Agakhan, Chama Cha madaktari, Saifee, Hospital binafsi na Hospital za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pia  miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni upimaji magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu, Saratani na magonjwa mengineyo hivyo tujitokeze kwa wingi kutumia fursa hii adhimu na ya kipekee ya kuimarisha afya zetu."

Sambamba na hilo "Serikali ya Awamu ya tano ya Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wawe na afya bora kwani ukiwa na afya bora utaweza kufanya kazi kwabidii na ndio maana Rais wetu amekua akiboresha huduma za afya na ujenzi wa vituo vya afya vya karibu na makazi ya wananchi ili kuweza kupata huduma kwa ukaribu zaidi hivyo niwaombe mzingatie mlo sahihi na pia muhakikishe elimu mtakayoipata hapa mnaemda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajafika waweze kufika kucheki afya zao kwani afya ni mtaji."Ameeleza Mheshimiwa Ludigija.

Aidha mheshimiwa Ludigija amewashukuru na kuwapongeza Wadau waliofanikisha zoezi Hilo ikiwemo  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na  Clouds Media group chini ya Mkurugenzi Joseph Kusaga, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Hospital ya Taifa Muhimbili, MOI, AghaKhan, PCMC, TMH, Chama Cha madaktari, Red Cross, hospital za Halmashauri ya Jiji ma Dar as Salaam, kampuni ya simu ya vodacom pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kufanikisha zoezi hili hivyo kuwaasa wananchi wajijengee utaratibu wakucheki afya zao mara kwa mara.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.