• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Halmashauri ya Jiji la DSM yafanya zoezi la usafi wa mazingira kanda namba moja

Tarehe iliyowekwa: August 31st, 2024

Katika kutekeleza agizo la Serikali la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi pamoja na kuendeleza na kutekeleza Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2024 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya  zoezi la usafi katika Kanda namba 1, usafi uliofanyika kwenye fukwe za Dengu kuelekea daraja la Tanzanite .

Akiongea wakati wa zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tarafa ya Kariakoo Bw. Adrian Kishe amewashukuru viongozi na wadau  wote walioshiriki zoezi la usafi huku akitoa wito kwa wananchi kufanya usafi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku .

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kuwa safi ili kuepukana magonjwa ya mlipuko. Hivyo na sisi tuhakikishe tunafanya usafi wa mazingira kila siku katika nyumba zetu na mitaa tunayoishi hivyo tusisubirie jumamosi ya mwisho wa mwezi tu”

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi ,  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu ameeleza kuwa “Halmashauri yetu imeazimia kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira bora na salama, Kama tunavyofahamu kuwa kiini cha magonjwa  ya milipuko chanzo ni uchafu wa mazingira yanayomzunguka. Endapo Mazingira Yatakua machafu , binadamu na viumbe hai vitaathirika, Kama ilivyo ada kila mwisho wa mwezi lazima tufanye usafi katika mazingira yetu hivyo sisi Halmashari tumefanya usafi hapa Dengu Beach ili kulinda afya za wananchi wetu na pia viumbe hai wanaishi baharini.”

Sambamba na hilo, ameeleza kuwa jukumu la kutunza mazingira ni la wananchi wote hivyo tuachane tabia ya kutupa taka  hivyo katika mazingira kwa ajili ya Afya zetu wenyewe na viumbe vinavyotuzunguka.

Aidha, Diwani wa Kata ya Kivukoni Mhe. Sharik Choughule amewapongeza na kuwashukuru viongozi, wadau, wananchi na taasisi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi katika beach hiyo.

“Mahali hapa ni sehemu mojawapo ambayo inatumiwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya mapumziko na mazoezi hivyo kwa kitendo hiki cha kusafisha mazingira haya ni kitendo cha uungwana na cha kuigwa, hivyo nitoe Shukrani zangu za dhati kabisa kwenu viongozi , wananchi na wadau wote kwa usafi mlioufanya." Amesema Mhe. Choughule.

Kwa upande wake Mkuu wa kanda namba moja Athumani Mtauka amesema kuwa jambo la usafi ni jambo la muhimu katika mazingira yetu  na Afya zetu na kuahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha mazingira yanakua safi na salama.







Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.