Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imenunua gari la kisasa la kubeba miili ya marehemu waliokosa ndugu ili kuweza kupelekwa katika makaburi kwa ajili ya shughuli za maziko.
Akizindua gari hilo jana Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles alieleza kwamba gari hilo jipya aina ya Isuzu lina thamani ya Shilingi Milioni Mia Moja (100 milioni) na lina uwezo wa kubeba miili ya marehemu minane (8) hadi kumi na sita (16) kwa wakati mmoja.
"Ndani ya gari hili kuna majokofu manne ambayo yatatumika kuilinda miili ya marehemu ili isiharibike na fedha zilizotumika kununua gari hili zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam", alisema Meya Mwita.
Tumejaribu mbadala wa kuwahifadhi ndugu zetu wale ambao hawana ndugu, kuna watu wanafariki katika hospitali zetu na kukosa ndugu wa kuwazika na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kutekeleza majukumu yake mojawapo likiwa ni utoaji wa huduma za maziko kwa maiti wasiokuwa na ndugu hivyo gari hili litatumika kuisitiri miili ya marehemu hao.
Mstahiki Meya ameeleza kwamba gari hilo litatumika kwa wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam na kwamba litakua na faida kwa wakazi wa Jiji ambao awali miili ilikuwa ikibebwa na malori.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.