Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya ziara ya kutembelea Soko la Samaki la Kimataifa la Feri kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mratibu wa Lishe Jijini Dar es Salaam Bi. Frola Mgimba amesema ameridhishwa na mazingira ya uandaaji wa samaki tangu hatua ya kwanza hadi kumfikia mlaji.
Awali Meneja wa Soko hilo Abdallah Mfinanga alisema Soko la Feri lina zaidi ya wafanyabiashara elfu tatu na linahudumia wateja zaidi ya elfu 12 kwa siku.
Soko hilo ambalo kihistoria lilianza mwaka 1950 wakati huo likiitwa Banda Beach ambapo ilipofika mwaka 1996 lilianza kujengwa na kukamilika 2002 na kuanza kuitwa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri baada ya kuhudumia mataifa mbalimbali.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.