• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

"Tutashirikiana na CRDB kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati" - DC Mpogolo

Tarehe iliyowekwa: June 22nd, 2025

Na: Doina Mwambagi

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, leo Juni 23, 2025 wameungana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea eneo litakapojengwa Shule ya Mfano ya Benki ya CRDB (CRDB Bank Model School), shule ya ghorofa nne inayotarajiwa kuwa ya kisasa zaidi jijini Dar es Salaam.

Shule hiyo mpya ya sekondari itakuwa na madarasa 16, maabara za kisasa 4, vyoo vya kisasa, na ofisi bora za walimu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuboresha mazingira ya ujifunzaji kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, amesisitiza  dhamira ya serikali kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ubora na uwazi.

“Tutashirikiana kwa karibu na CRDB Benki kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika ipasavyo, kwa ubora unaostahili na kwa wakati uliopangwa. Serikali ya Wilaya itahakikisha kuwa thamani ya mradi huu inaendana kikamilifu na fedha zinazowekezwa,” ameeleza  Mpogolo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, ameeleza  kuwa mradi huo ni zawadi kwa vizazi vijavyo na ni kielelezo cha ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na serikali.

“Mradi huu wa shule ya mfano unaakisi dhamira ya kweli ya kuwekeza kwenye kizazi cha sasa kwa ajili ya Tanzania ya kesho. Tunapongeza CRDB na Mbunge wa Ilala kwa kujitoa na kushirikiana nasi katika kuinua sekta ya elimu,” alisema Mabelya.

Mkurugenzi Mabelya ameongeza kuwa hadi sasa Jiji lina jumla ya shule 118, na Shule ya Mfano ya CRDB itakuwa ya 119. Ameeleza kuwa kuna uhitaji mkubwa wa uwekezaji zaidi katika sekta ya elimu ili kufikia matokeo chanya, na kwamba mradi huo unakwenda sambamba na sera ya uwekezaji kwa jamii, hivyo Halmashauri inajivunia kuwa sehemu ya utekelezaji wake.

Mradi huu unakwenda sambamba na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwekeza kwa dhati katika sekta ya elimu kupitia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.










Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutashirikiana na CRDB kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati" - DC Mpogolo

    June 22, 2025
  • Naibu Spika atembelea eneo la ujenzi wa shule ya mfano ya CRDB

    June 22, 2025
  • Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa kutoa elimu ya mikopo ya asilimia 10 - DC Mpogolo

    June 20, 2025
  • "Mikopo ya asilimia 10 ni silaha ya kuinua uchumi wa wananchi" - DC Mpogolo

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.