JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Tarehe: 31 March, 2016

Mahali: City Hall

Muda: 08:00 - 15:00

Maelezo Ya Tukio:

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM 

KUWASILISHA TAARIFA ILI KUWEZESHA MALIPO KWA NJIA YA MFUMO WA MALIPO WA KIELEKTRONIKI SERIKALINI 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anapenda kuwajulisha wadau wote kwamba kuanzia mwezi Aprili, 2016 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itafanya malipo moja kwa moja katika akaunti za walipwaji kwa kupitia mtandao wa malipo wa Benki Kuu ya Tanzania “Tanzania Interbank Settlement System (TISS)”.

Taarifa zinazohitajika ili kuwezesha malipo kwa mlipwaji ni pamoja na hizi zilizoorodheshwa hapa chini:

  1. Namba ya akaunti ya benki.
  2. Namba ya tawi la benki (Branch Code-Bic Number)
  3. Jina la akaunti
  4. Aina ya akaunti (Account Type)
  5. Namba ya kuandikishwa biashara (Business Registration Number)
  6. Namba ya kuandikishwa Kampuni (Company Registration Number)
  7. Namba ya Mlipakodi (Tax Identification number-TIN)
  8. Jina la benki.
  9. Jina la Tawi la benki.


Hivyo kwa tangazo hili makampuni na watu wanaofanya biashara au kutoa huduma kwa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam mnapaswa kufika ofisi ya Halmashauri ya Jiji, City Hall ili kupata fomu maalum ya kujaza taarifa hizo muhimu.


Bonyeza hapa kupakua fomu tajwa.


Wilson M Kabwe

MKURUGENZI WA JIJI

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM