Jiji la Dar es Salaam na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania wamesaini Hati ya makubaliano ya awali ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuweka miundombinu ya kudhibiti taka ngumu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Hati hiyo ya makubaliano hayo ya awali ilisainiwa Novemba 21 mwaka huu na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa ya Ubungo, Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni.
Mafanikio haya yanatokana na kikao kilichofanyika tarehe 05 Septemba, 2017 kati ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora J. Liana pamoja na wataalam kutoka OR-TAMISEMI na wageni kutoka Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania wakiwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Miundominu na Mazingira ya nchini Uholanzi ili kujadili kwa pamoja namna bora ya usimamizi wa taka ngumu zinazozalishwa jijini Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.