JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji kujadili bajeti ya 2017/2018

Bajeti ya Halmashauri ya Jiji katika mwaka 2017/2018 imeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo 2025, malengo endelevu ya millennia, Mpango wa maendeleo wa miaka mitano (5), Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2017/2018 na maelekezo mengine ya Serikali na Halmashauri ya Jiji. Bajeti hii imejikita katika kumalizia miradi inayoendelea na kutekeleza miradi mipya ambayo inaleta tija kwa wananchi wa Dar es Salaam. Aidha bajeti ya Halmashauri imezingatia vipaumbele vifuatavyo:

 • Kuboresha mapato ya Halmashauri kwa kupitia upya sheria ndogo na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
 • Ujenzi na ukarabati wa majengo, barabara na vituo vikuu vya mabasi yaendayo mikoani (Mbezi Luis na Boko)
 • Kuboresha eneo la kutupa taka kitaalam – (Sanitary Landfill) kwa kujenga ukuta, kununua mitambo ya kusukuma na kushindilia taka, kujenga barabara za ndani na mfumo wa kamera za Usalama (CCTV)
 • Uwekezaji vitega uchumi kwenye viwanja vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Appartments)
 • Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa utoaji wa huduma (supportive supervisión) kwenye Halmashauri na Hospitali za Rufaa za Mikoa (Regional Referal Hospitals).
 • Kuratibu na kufuatilia uboreshaji wa huduma ya uzazi na mtoto hususan kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga
 • Kuratibu mikakati ya utekelezaji wa shughuli za kudhibiti magonjwa ikiwemo UKIMWI, Kifua kikuu, malaria na magonjwa yasiyoambukiza
 • Kununua maeneo kwa ajili ya uwekezaji na kupima viwanja kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri
 • Kusimamia uendelezaji wa makazi na matumizi ya ardhi. Kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dar es Salaam kwa kufanya uhamasishaji kwa viongozi wa kata, mitaa na jamii kwa ujumla
 • Uendelezaji wa Utalii, hifadhi ya mazingira na kuviwezesha vikundi vya akina mama na vijana.
 • Kufanya utafiti unaohusu usindikaji wa taka kwa kuwasilisha kwa njia ya maonesho pamoja na kuelimisha umma namna ya kurejeleza taka na kuwa bidhaa. 

Makisio ya bajeti ya mwaka 2017/2018 ni jumla ya Sh. 20,278,441,110.00 ambapo Sh. 3,133,512,000.00 ni Ruzuku toka Serikali Kuu na Sh. 17,144,929,110.00 ni makusanyo ya ndani. Aidha, kati ya mapato haya kiasi cha Sh. 6,674,688.000 ni mapato ya kugawana na Halmashauri za Manispaa na hivyo jumla ya Sh. 10,470,241,110.00 ni mapato ya ndani yatakayotumika kugharimia matumizi ya kawaida yaani matumizi mengineyo (OC), mishahara ya watumishi (PE) pamoja na miradi ya maendeleo. Jumla ya Sh. 3,377,789,976.00 zitatumika kulipia matumizi mengineyo (OC) na Sh. 530,360,968.00 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi, Aidha Sh. 6,562,144,166.00 zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 62.67 % ya mapato yote ya ndani.   


Na.

Mchanganuo

Jumla

1

Jumla ya Mapato

17,144,929,110.00

2

Mapato ya Kugawa kati ya Manispaa na Wakala.

6,674,688,000.00

3

Mapato ya Ndani

10,470,241,110.00

4

Mishahara ya Ndani

530,360,968.00

3

Matumizi ya Kawaida

3,377,789,976.00


Miradi ya maendeleo vyanzo vya ndani


1

Ufuatiliaji na Tathmini (M & E)

293,107,208.30

2

Ukarabati wa barabara ya  kuingia/kutoka dampo kwa kiwango cha lami yenye urefu wa 0.7km

600,000,000.00

3

Kukamilisha ujenzi wa ukuta wa kuzunguka Dampo (920m)

320,000,000.00

4

Ukarabati wa barabara za Dampo la Pugu Kinyamwezi

100,000,000.00

5

Kulipa fidia na kujenga miundombinu ya Dampo la Mkuranga na Kigamboni

1,000,000,000.00

6

Ununuzi wa maeneo na ujenzi wa vyoo vya umma

500,000,000.00

7

Mchango wa ujenzi wa kituo cha Mbezi Luis

1,035,000,000.00

8

Ukarabati wa majengo Halmashauri ya Jiji (DCC)

210,229,411.00

9

Kufunga camera za  CCTV katika jengo kuu la Halmashauri  ya jiji

50,000,000.00

10

Ujenzi wa vyoo vya umma na kukarabati mfumo wa umeme Karimjee Hall

162,447,546.70

11

Ukarabati wa miundombinu kituo cha mabasi  Ubungo

200,000,000.00

12

Kununua eneo kwa ajili ya makaburi

300,000,000.00

13

Kodi ya viwanja vya Halmashauri (Land Rent)

250,000,000.00

14

Mikopo kwa jamii (vijana na wanawake)

977,000,000.00

15

Matengenezo ya mzani Dampo la Pugu Kinyamwezi

10,000,000.00

16

Matengenezo ya Mitambo ya kusukuma na kushindilia taka.

150,000,000.00

17

Gharama za uendeshaji dampo (Diesel na Petrol)

404,360,000.00


Jumla miradi ya maendeleo

6,562,144,166.00

2

Ruzuku ya Serikali Kuu


2.1

Mishahara

2,275,512,000.00

2.2

Matumizi ya Kawaida

-

2.3

Miradi ya Maendeleo ya Ruzuku LDGD

850,000,000.00

2.4

Kuthibiti UKIMWI (NMSF)

8,000,000.00


Jumla ndogo ya Ruzuku

3,133,512,000.00


Jumla kuu

20,278,441,110.00