JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Mafunzo ya Kanuni za uendeshaji wa Halmashauri ya Jiji

Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 06 Machi, 2017 wakiwa katika mafunzo ya Kanuni za uendeshaji wa Halmashauri ya Jiji.

Mafunzo hayo yatawawezesha Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba, Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Kitaifa na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora na maendeleo kwa wananchi.